Kutana na Kijana Anaishi Kwenye Maji Muda Wote Kama Mamba, Kisa Kizima Hichi Hapa

Iqbal Sheikh
Iqbal Sheikh

Kutana na Kijana Anaishi Kwenye Maji Muda Wote Kama Mamba, Kisa Kizima Hichi Hapa

Katika kijiji cha Beldanga, kilichopo Wilaya ya Murshidabad nchini India, kuna kisa cha kusikitisha na kinachovuta hisia cha kijana mwenye umri wa miaka 16, Iqbal Sheikh. Kwa miaka mitano sasa, Iqbal anajikuta katika hali isiyo ya kawaida inayomfanya atumie siku kadhaa akikaa ndani ya mabwawa bila kutoka.

Maumivu Makali Yanayomfukuza Nchi Kavu Kwa kijana huyo, kutoka nje ya maji ni sawa na kuingia kwenye moto. Mara tu ngozi yake inapokutana na hewa ya nchi kavu, huanza kuhisi maumivu makali sana ya kuungua, kizunguzungu na kupoteza uwezo wa kuona vizuri. Hali hiyo humlazimu kurejea majini ili kupata nafuu.

  • Kula na Kuishi Majini: Kutokana na maumivu hayo, Iqbal hulazimika kula biscuits na vyakula vyepesi akiwa ndani ya maji.

  • Imani za Kienyeji na Hofu: Kijana huyo amewahi kuamini kuwa amevamiwa na jini anayemlazimisha kukaa majini, kutokana na ukosefu wa majibu ya kitabibu kwa muda mrefu.

Madhara ya Afya Kupitiliza Licha ya maji kumpa nafuu ya muda, kukaa humo mchana na usiku kwa siku kadhaa mtawalia kunaweka afya yake hatarini zaidi. Ngozi yake imeanza kubadilika rangi kuwa nyeupe na kulainika kupitiliza (maceration), huku akipata maambukizi ya mara kwa mara ya mafua na kifua. Madaktari wanaonya kuwa hali hiyo inaweza kusababisha maambukizi makubwa ya bakteria na fangasi kwenye ngozi.

Matumaini Mpya na Hatua za Kitabibu Baada ya video za Iqbal kusambaa kwa kasi mtandaoni, kisa chake kimepata usikivu wa kitaifa. Kupitia msaada wa wadau na taasisi za kiutu, Iqbal amesafirishwa hadi jijini Mumbai katika Hospitali ya Sir HN Reliance Foundation kwa ajili ya vipimo vya kina.

Madaktari wanachunguza uwezekano wa matatizo ya mfumo wa neva na ngozi, ikiwemo ugonjwa nadra uitwao Erythromelalgia au Anhidrosis unaoathiri uwezo wa mwili kudhibiti joto na maumivu. Pamoja na kwamba uchunguzi bado unaendelea, familia yake ina matumaini makubwa ya kupata tiba sahihi itakayomrejesha Iqbal katika maisha ya kawaida ya nchi kavu.

Related Posts