Jeshi la Polisi Lathibitisha Kumkamata Godlisten Malisa na Kumwachia Kwa Dhamana

Godlisten Malisa
Godlisten Malisa

Jeshi la Polisi Lathibitisha Kumkamata Godlisten Malisa na Kumwachia Kwa Dhamana

Jeshi la Polisi Mkoani Arusha limethibitisha kuwa jana Agosti 31, 2026 majira ya usiku lilimkamata Godlisten Elisante Malisa akiwa na mwenzake kutokana na tuhuma za jinai zilizokuwa zinachunguzwa dhidi yake.

Kwa mujibu wa taarifa ya leo Septemba Mosi, 2026 iliyotolewa na Kamanda wa Polisi Mkoa wa Arusha, Malisa na mwenzake walifanyiwa mahojiano na kuachiwa kwa dhamana wakisubiri taratibu zingine za kisheria kukamilishwa.

Taarifa ya Jeshi la Polisi imekuja saa kadhaa baada ya Mtandao wa Watetezi wa Haki za Binadamu Tanzania (THRDC) kutoa wito kwa Jeshi la Polisi na ldara ya Uhamiaji kueleza mahali Malisa alipokuwa akishikiliwa na sababu za hatua hiyo.

ALSO READ | Ukweli Kuhusu Tukio la Ndege Iliyopotea Angani na Kurudi Tena Duniani Baada Ya Miaka 35

Related Posts