
VIDEO: Mwanafunzi Ajirusha Ghorofani Loreto Mwanza, Polisi Wafunguka Kilichotokea
Jeshi la Polisi Mkoa wa Mwanza limesema linaendelea na uchunguzi wa kifo cha Stellah Wangaluke Shilingi (15), Mwanafunzi wa Kidato cha Tatu katika Shule ya Sekondari ya Wasichana Loreto anayedaiwa kujirusha kutoka ghorafani huku akiacha ujumbe.
Stellah alifariki Agosti 31, 2026 baada ya kupata majeraha akiwa shuleni katika eneo la Majengo Mapya, Kata ya Nyakato, Wilaya ya Ilemela, Mkoani Mwanza.
Baada ya tukio hilo, Mwanafunzi huyo alikimbizwa Hospitali ya Rufaa ya Kanda Bugando kwa ajili ya matibabu, lakini alifariki dunia baada ya kufikishwa hospitalini hapo.
Kwa mujibu wa Jeshi la Polisi, uchunguzi wa awali umehusisha tukio hilo na msongo wa mawazo, huku uchunguzi zaidi ukiendelea ili kubaini mazingira kamili ya kifo chake.
View this post on Instagram
ALSO READ | Mashabiki wa Timu ya Simba Wamliza Mchezaji Ibrahim Doumbia
