
Mashabiki wa Simba Wasiingie Kwenye Mtego: Doumbia Anahitaji Subira, Siyo Presha
Ushindi wa mabao 6-1 wa Simba SC dhidi ya Mighty Wanderers katika Ligi ya Mabingwa Afrika ulikuwa ni wa kishindo, lakini mjadala uliotawala baada ya mchezo huo umeelekeza mshale kwa mshambuliaji Doumbia kufuatia ukame wake wa kufunga. Ni jambo la kawaida kwa mshambuliaji yeyote bora kupitia kipindi kigumu cha ukame uwanjani, na hilo haliondoi ubora wake kama mchezaji.
Wakati wapinzani wakitumia fursa hiyo kuhamisha umakini kutoka kwenye ushindi mnono wa Simba na kuangazia kutokufunga kwa Doumbia, baadhi ya mashabiki wa Simba wameingia kwenye mtego huo kwa kuanza kumshambulia mchezaji wao. Wanasiha na wadau wa soka wanaeleza kuwa mshambuliaji huyo anahitaji kuungwa mkono na kupewa muda, kwani uwezo anao na siku yake ya kuanza kucheka na nyavu haipo mbali.
Shaffih Dauda
