Mwanamke Akamatwa Akimpelekea Mpenzi Wake Bangi Iliyofichwa Kwenye Mkate Mahabusu

Mwanamke Akamatwa Akimpelekea Mpenzi Wake Bangi Iliyofichwa Kwenye Mkate Mahabusu
Mwanamke Akamatwa Akimpelekea Mpenzi Wake Bangi Iliyofichwa Kwenye Mkate Mahabusu

Mwanamke Akamatwa Akimpelekea Mpenzi Wake Bangi Iliyofichwa Kwenye Mkate Mahabusu

DAR ES SALAAM — Mwanamke mmoja mwenye umri wa miaka 26, Bernice Achieng, amekamatwa nchini Kenya baada ya polisi kumkuta na kete 12 za bangi, tano kati yake zikiwa zimefichwa kwa ujanja ndani ya mkate aliokuwa amempelekea mpenzi wake aliyekuwa akishikiliwa katika Kituo cha Polisi Buruburu, Nairobi.

Taarifa iliyotolewa na Kurugenzi ya Upelelezi wa Jinai nchini Kenya (DCI) inaeleza kuwa tukio hilo limetokea leo Jumatatu, Septemba 21, 2026, baada ya Achieng kufika kituoni hapo kumtembelea mpenzi wake.

Jinsi Ugunduzi Ulivyofanyika

Kwa mujibu wa mtandao wa Capital FM, Achieng aliwaomba maofisa waliokuwa katika dawati la taarifa wamkabidhi mpenzi wake mkate aliotembea nao. Hata hivyo, maofisa hao walitilia shaka kifurushi hicho baada ya kubaini kuwa hakikuwa kimefungwa vizuri, hatua iliyowafanya wakikague.

Katika upekuzi huo, polisi walikuta kete tano za bangi pamoja na kiboksi cha kiberiti vikiwa vimefichwa ndani ya mkate huo.

“Baada ya ugunduzi huo, Achieng alifanyiwa upekuzi zaidi, ambapo polisi walidai kukuta kete nyingine saba zilizokuwa zimefichwa kwenye mfuko wa koti lake,” imeeleza taarifa ya DCI.

Achieng anaendelea kushikiliwa na jeshi la polisi huku vielelezo vyote vilivyokamatwa vikihifadhiwa kwa ajili ya hatua za kisheria.

Kete 300 Zingine Zakamatwa Thika

Katika hatua nyingine, polisi nchini Kenya wamemkamata mwanaume mmoja anayedaiwa kujihusisha na usambazaji wa dawa za kulevya katika eneo la Kairi, Thika West.

DCI imemtaja mshukiwa huyo kuwa ni John Mwangi, maarufu kama ‘Bombay’, ambaye alikuwa akisafiri kwa pikipiki akiwa amempakia mwanamke mmoja. Wawili hao walijaribu kukwepa kizuizi cha polisi kwa kuongeza mwendo, lakini polisi waliwafuatilia hadi karibu na Ree Supermarket ambapo Mwangi aligonga kituta cha barabarani na kuanguka.

Baada ya ajali hiyo, abiria wa kike aliyekuwa naye alifanikiwa kutoroka na kutoweka kwenye umati wa watu, huku Mwangi akikamatwa papo hapo. Upekuzi kwenye pikipiki hiyo ulisababisha kukamatwa kwa kete 300 za bangi na kilo tatu za bangi zilizokuwa zimehifadhiwa chini ya kiti cha pikipiki.

Mwangi anashikiliwa katika Kituo cha Polisi Kimuchu akisubiri kufikishwa mahakamani.

DCI imebainisha kuwa operesheni hizo mbili zimesababisha kukamatwa kwa jumla ya kete 312 za bangi na kilo tatu za bangi zikiwa ni juhudi za kuendelea kupambana na usambazaji wa dawa za kulevya.

Related Posts