
Timu ya Taifa ya vijana ya Tanzania U-20, Ngorongoro Heroes imepoteza kwa penalti 4-3 dhidi ya Sudan kwenye fainali ya michuano ya kuwania kufuzu Kombe la Mataifa Afrika kwa wachezaji wa umri chini ya miaka 20, AFCON U-20 2027 kwa ukanda wa CECAFA.
Hata hivyo tayari Tanzania pamoja ma Mwanafainali mwenzake, Sudan ambao ndio Mabingwa wa CECAFA U-20 wamekata tiketi ya kushiriki michuano ya AFCON U-20 2027 itakayofanyika Nchini Ghana mwaka 2027.
FT: Sudan U-20 🇸🇩 1-1 🇹🇿 Tanzania U-20 (P 4-3)
⚽ 92’ Omer Ahmed
⚽ 111’ Abdulnassir ‘Casemiro’
