BASATA Yawashushia Rungu Dudubaya na Mratibu wa Tamasha la Miaka 30 ya Bongo Flava

Dudubaya
Dudubaya

BASATA Yawashushia Rungu Dudubaya na Mratibu wa Tamasha la Miaka 30 ya Bongo Flava

Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA) limemchulia hatua za kinidhamu msanii nguli wa muziki nchini, Godfrey Tumaini maarufu kama Dudubaya, pamoja na Mratibu Mkuu wa Tamasha la Miaka 30 ya Bongo Flava kufuatia ukiukaji wa maadili wakati wa tamasha hilo lililofanyika Septemba 19, 2026, katika Viwanja vya General Tyre, Jijini Arusha.

Kwa mujibu wa taarifa rasmi kutoka BASATA, Dudubaya alikiuka Kanuni ya 20(a) ya Kanuni za Baraza la Sanaa la Taifa (Tangazo la Serikali Na. 137 la tarehe 22 Mei 2026) kwa kutumia lugha ya matusi na kashfa jukwaani akiwa anatumbuiza.

Muhtasari wa Adhabu Zilizotolewa:

1. Godfrey Tumaini (Dudubaya)

  • Kosa: Kutumia maneno ya kashfa na matusi yanayokiuka maadili ya sanaa nchini akiwa jukwaani.

  • Adhabu:

    • Kulipa faini ya TSh 3,000,000 ndani ya siku 14 kuanzia tarehe ya uamuzi.

    • Kufungiwa kujishughulisha na kazi za sanaa kwa namna yoyote ile hadi pale atakapotekeleza kikamilifu masharti ya adhabu hiyo.

    • Kutakiwa kuzingatia sheria, kanuni na miongozo ya BASATA katika shughuli zake za sanaa.

2. Mratibu Mkuu wa Tamasha la Miaka 30 ya Bongo Flava

  • Kosa: Kushindwa kusimamia na kudhibiti mwenendo wa tamasha, na kumruhusu msanii kufanya ukiukaji wa maadili jukwaani kinyume na masharti ya kibali cha maandalizi.

  • Adhabu:

    • Kulipa faini ya TSh 3,000,000 ndani ya siku 14 kuanzia tarehe ya uamuzi.

    • Kufungiwa kuratibu au kujishughulisha na matukio ya sanaa hadi atakapotekeleza maamuzi ya Baraza.

    • Kupewa maelekezo ya kuzingatia miongozo ya uendeshaji wa matukio ya sanaa nchini.

BASATA imewakumbusha wasanii, waandaaji na wadau wote wa sekta ya sanaa nchini kuhakikisha wanafuata Sheria, Kanuni, Miongozo na Maadili ya Kitanzania wakati wote wanapotekeleza kazi zao

Related Posts