Zitto Kabwe Achafukwa “Mnajadili Kuhusu Jezi Mnaisahau Taifa Stars, Ndio Maana Mmefungwa”

Ameandika Zitto Kabwe kupitia Instagram;

Benard Kamungo Mshambuliaji wa FC Dallas ya Marekani ambaye amecheza Timu ya Taifa ya USA ya under 20 kaamua aipe heshima Nchi ambayo imemlea, Tanzania. Kakubali kujiunga na Taifa Stars. TFF wamefanya kazi yao na wamemleta. Kwa furaha kajiunga na Kambi ya Timu ya Taifa. First 11 imetoka hayupo hata kwenye Subs. Kisa? Serikali ya Tanzania haijampa Pasipoti. Nchi nzima inajadili JEZI! Uzuri au ubaya wa Jezi lakini hatuna muda kabisa wa kufanya mambo muhimu.

Tunajadili Petty Issues na kuacha mambo ya kimkakati. Waziri wa Michezo anashinda kwenye Press kuelezea ubaya au uzuri wa Jezi ilhali angehitaji saa moja tu kuhakikisha mchezaji muhimu kabisa anapata Pasipoti. Waziri wa Ndani anaita wasanii ofisini kukata kesi, Waziri wa Mambo ya nje hata Sijui yupo wapi, Waziri wa Michezo analilia dili la jezi. Timu imeachwa! Ndio maana inafungwa hata na Timu ya 132 kwenye FIFA RANKING. Waziri @baba_keagan achana na mambo ya jezi focus on our team. Waziri Mahmoud Kombo na Waziri Katambi Timu inakwenda Morocco katika siku mbili hakikisheni suala la Kamongo limekwisha. Hebu tuwage serious na mambo ya Nchi

Kabla ya Mechi Zitto Aliandika Haya:

Kesho nitakuwa uwanjani kuwapa support Taifa Stars. Nitavaa Jezi Rasmi ya Taifa Stars ambayo ni hii. Hakuna Jezi nyengine zaidi ya hii. Nilizungumza na Waziri @baba_keagan kuhusu huu mjadala wa Jezi na nikwamwambia ni mjadala hauna maana kabisa. Alinipa maelezo yake na nikwambia baadhi ni maelezo mazuri kabisa lakini yanapaswa kujadiliwa mezani na kelele mitaani. Nilizungumza na watu wa sandaland pia na kuwaambia wanapaswa kukaa na Wizara ili kuchukua mawazo yao. kutaka NIKE wauze jezi zetu Haina shida, NIKE wanunue rights kutoka Sandaland. Uongozi unataka kutoa empowerment kwa wananchi wako. Kama Sandaland tayari Ana mkataba na TFF. Halafu tumewapata NIKE hakuna shida. Waziri angemsaidia Mtanzania kuhamisha rights kwa NIKE ambapo Taifa lingefaidika na Mtanzania angefaidika sana. Waziri kutangaza kuwa jezi mbaya inaonyesha kuwa hakai wizarani na hafuatilii kazi zake za uwaziri. Jezi ambayo tayari Timu ya Taifa inavaa unatangazaje kuwa ni mbaya? Timu inacheza kesho na ipo kwenye ratiba badala ya ku focus kwenye ushindi wa Timu tunahamisha mjadala kwenye jezi. Mchakato wa Jezi ni mrefu, Waziri kulalamika mtaani ni kushindwa uongozi. Narudia Waziri Makonda na kampuni ya sandaland waachane na huu mjadala usio na maana yeyote. Huu ni mjadala wa watu walioshiba. Ni mjadala unaondoa focus kwa Timu. Mambo yote Waziri anataka yanaweza kuboreshwa kwa kukaa na Sandaland. Waziri amefanya kosa kubwa kuukuza Huu ugomvi usio na maana kabisa. @baba_keagan weka mawe mfukoni tafadhali. Elekeza nguvu kwenye kuboresha tufanye vizuri. @sandaland_theonlyonetz achana na mambo ya mahakamani. Kaeni chini na Waziri kupata jawabu. Mkataba wa kuzalisha Jezi ni halali na unapaswa kutekelezwa. Ubora wa jezi ni jambo la kuboresha na sio jambo la kelele za mtaani. Kuendeleza mjadala Huu ni ku JINX national team. Kama Waziri Makonda anao NIKE awaite waongee na Sandaland kisheria ili kuhamisha rights commercially. Kutaka kutafuta sababu za kipuuzi kumnyanganya mkataba sandaland ni UZWAZWA na UNDEZI wa Hali ya Juu sana. Unamnyanganya vipi MZAWA mwenye mkataba na kumpa mgeni badala ya kumwunganisha huyo mzawa na Nike? Hizo hazitakuwa akili itakuwa ni Matope yamekaa kichwani tu

Related Posts