Mama Mzazi wa Jihan Dimack Ajitokeza na Kuelezea Uraia wa Mwanaye

 

Mama Mzazi wa Jihan Dimack Ajitokeza na Kuelezea Uraia wa Mwanaye
Mama Mzazi wa Jihan Dimack Ajitokeza na Kuelezea Uraia wa Mwanaye

Mama Mzazi wa Jihan Dimack Ajitokeza na Kuelezea Uraia wa Mwanaye

Mama Mzazi wa Jihan Dimack, mshindi wa taji la Miss Grand International 2026, amesisitiza kuwa Mwanaye ni Mtanzania mwenye asili ya Kisukuma, aliyezaliwa na kusoma Mkoani Mwanza, huku akieleza kuwa uwezo wake wa kuzungumza Kiingereza haupaswi kuwafanya Watu kuwa na mashaka kuhusu asili yake.

Akizungumza na Waandishi wa Habari leo, Oktoba 19, 2026, Mama huyo amesema, “Mwanangu kazaliwa na kusoma Mwanza, ni Msukuma, labda kile Kiingereza ndiyo kinawachanganya.”

Aidha, amefunguka kuhusu hisia alizopitia wakati Jihan akitangazwa Mshindi wa taji hilo Nchini Thailand, akisema alilia kwa nguvu na kubaki amezubaa kutokana na furaha na mshangao.

Amesema wakati huo presha yake ilipanda na mwili wake kuvimba, huku akieleza kuwa safari yao nchini Thailand ilikuwa na changamoto nyingi, ikiwemo kukesha usiku na kupata muda mchache wa kupumzika.

Related Posts