Mhubiri Paul Mackenzie Akutwa na HATIA Kuuwa Wafuasi Wake 191 Msitu wa Shakahola

Mahakama Kuu Jijini Mombasa Nchini Kenya, leo Oktoba 19, 2026, imemkuta na hatia Mhubiri Paul Mackenzie pamoja na wenzake 28 kwa makosa ya mauaji ya Watu 191, wakiwemo Watoto 190 na Mtu mmoja mzima, katika tukio lililohusishwa na mafundisho ya kidini kwenye Msitu wa Shakahola.

Akitoa uamuzi huo, Jaji Diana Kavedza amesema Upande wa Mashtaka umefanikiwa kuthibitisha makosa dhidi ya Washtakiwa hao bila kuacha shaka yoyote, baada ya Mahakama kupitia ushahidi uliowasilishwa kuhusu vifo hivyo.

Kutokana na hatua hiyo, Mahakama imepanga kupokea taarifa za maandalizi ya adhabu Oktoba 30, kabla ya kutangaza adhabu dhidi ya waliopatikana na hatia Novemba 6, 2026.

Tangu mwaka 2023, mamia ya miili imepatikana ikiwa imezikwa katika makaburi ya pamoja ndani ya Msitu wa Shakahola, Kaunti ya Kilifi, ambapo Mackenzie anadaiwa kutumia mafundisho ya kidini kuwashawishi Waumini wake kufunga kula hadi kufa kwa imani kwamba wangekutana na Yesu.

Related Posts