SIMBA Yabonda Mtu 6 – 1, Doumbia Atupia, Haya Ndio Yaliyojiri

SIMBA Yabonda Mtu 6 - 1, Doumbia Atupia, Haya Ndio Yaliyojiri
SIMBA Yabonda Mtu 6 – 1, Doumbia Atupia, Haya Ndio Yaliyojiri

Anaandika @kelvinrabson_

✍🏼 Mechi ambayo ilikuwa ya upande mmoja kwa muda mrefu , Simba walikuwa perfect wakiwa na umiliki wa mpira na bila mpira …. Kivipi ?

A) WAKIWA NA MPIRA WANAFANYA NINI ?

✍🏼 Wanaonekana wapo sharp na fit zaidi kwenye matukio ya mpira : wanahakikisha kila eneo ambapo kuna mpira wanatengeneza idadi kubwa ya wachezaji ( Create Overlords ) rahisi kwao kuunganisha pasi kusogea juu .

✍🏼 Eneo la pembeni ya kiwanja wanakuwa na muunganiko mzuri ( Fullbacks & wingers ) Chilambo na Mlingo wanashambulia nafasi eneo la ndani “ half spaces “ then Libase na Oura wanakuwa pembeni zaidi dhumuni ni kutengeneza 1 vs 1 dhidi ya fullbacks wa De Agosto ( walifanikiwa na ndio goli la kwanza limetokea kwenye move hiyo )

✍🏼 Level ya kiufundi kwa wachezaji wa Simba ilikuwa kubwa zaidi ya De Agosto wanakuwa na umiliki mkubwa wa mchezo , wanapasiana vizuri , runs za kutosha na wanatunza mali vizuri .

✍🏼 Rotation na movements ya wachezaji kuharibu muundo wa ulinzi wa De Agosto na kwenye nyakati nyingi wanaonekana kuwa na idadi kubwa ya wachezaji .

B) BILA MPIRA WANAFANYA NINI ?

✍🏼 Wanaweka presha haraka kwenye mpira na kwa mpinzani dhumuni kurudisha umiliki na kulazimisha turnovers .

✍🏼 Distance ndogo sana kati ya mstari mmoja na mwingine ndio maana ilikuwa ngumu kwao kutupa mipira kirahisi .

✍🏼 15 De Agosto mkakati wao wa kuzuia eneo la chini lilikuwa sahihi tatizo ni utekelezaji wake ndio haukuwa sawa : wanapoteza mpira kirahisi , wakiwa na mpira hakuna idea yeyote then kuna nafasi kubwa kati ya mchezaji mmoja na mwingine .

NOTE :

1: Nathaniel Chilambo amefanya kazi nzuri sana kwenye kuzuia na amehusika kwenye goli .

2: Libasse na Oura wanatoa msingi sahihi kwa Simba kuifungua defense ya mpinzani .

3: Doumbia alihitaji atleast goli kurudisha confidence yake .

4: Mpanzu kaubonda sana ngumu kukabiliana nae .

5: Maema mtu sana akiwa na mpira mguuni ngumu kupoteza , anaifanya timu itembee kwa haraka .

FT : 15 De Agosto 1-6 Simba

Related Posts