
Yanga Yatinga Makundi kwa Kishindo, Yaichapa CFFA 8-1 kwa Jumla
DAR ES SALAAM: Klabu ya Yanga SC imefanikiwa kutinga hatua ya makundi baada ya kuichapa CFFA FC mabao 4-1 katika mchezo wa marudiano uliopigwa Oktoba 21, 2026, kwenye Uwanja wa Azam Complex.
Matokeo hayo yanaifanya Yanga kusonga mbele kwa ushindi wa jumla ya mabao 8-1, baada ya kuendelea kuonyesha makali yake katika michuano hiyo.
Katika mchezo huo, Ibrahim Kazimoto alianza kuandika historia ya mabao kwa kuifungia Yanga bao la kwanza dakika ya 27, akimalizia pasi ya Mudathir Yahya.
Kipindi cha pili kilianza kwa kasi kwa upande wa Yanga, huku Seleman Mwalimu akifunga mabao mawili ndani ya dakika nne, akitikisa nyavu dakika ya 48 na 52 na kuifanya timu yake kuongeza faida.
CFFA FC ilipata bao lake pekee dakika ya 74 kupitia Fitahianstoa Albertini, aliyefunga kwa mpira wa adhabu ndogo akiwa nje ya eneo la hatari la mita 18, akimshinda kipa wa Yanga, Aboutwalib Mshery.
Hata hivyo, Yanga haikuishia hapo, kwani Chuga alifunga bao la nne dakika ya 83 na kukamilisha ushindi wa mabao 4-1 katika mchezo huo.
Ushindi huo unaipa Yanga nafasi ya kuendelea na safari yake katika mashindano hayo, huku ikisubiri kujua wapinzani wake katika hatua ya makundi.
Katika mchezo huo, Yanga ilianza na kikosi kilichokuwa na Aboutwalib Mshery langoni, akisaidiwa na Ibrahim Kazimoto, Boka, Komara na Bakari Nondo katika safu ya ulinzi.
Eneo la kiungo lilikuwa na Ngoma, Mudathir Yahya na SureBoy, huku Toure, Seleman Mwalimu na Albert Kangwanda wakiongoza safu ya ushambuliaji.
Wachezaji waliokuwepo benchi la akiba ni Masalangwa, Job, Hussein, Mussa, Maxi Nzengeli, Abushiri, Zakouani, Aziz Ki na Mzize.
Kwa matokeo hayo, Yanga imehitimisha hatua hiyo kwa ushindi wa jumla wa mabao 8-1 dhidi ya CFFA FC na kuweka matumaini mapya kwa mashabiki wake kuelekea hatua ya makundi.
