
JESHI la Polisi Tanzania limesema limebaini mipango ya kufanya vurugu, kuharibu miundombinu na mali za umma na binafsi, likisisitiza kuwa wanaohusika watachukuliwa hatua za kisheria.
Katika taarifa iliyotolewa Oktoba 26, 2026 na Msemaji wa Jeshi la Polisi Tanzania David Misime amesema baadhi ya viongozi wa dini, siasa na wanaharakati wanahusishwa na matamko na mipango inayolenga kuwashawishi wananchi kujiingiza katika vitendo vya kihalifu.
Amesema Jeshi la Polisi linaendelea kushirikiana na vyombo vingine vya ulinzi na usalama kufuatilia mipango hiyo na kubaini wahusika.
Aidha, jeshi hilo limewataka wananchi kuzingatia sheria za nchi, kulinda amani na kutoa taarifa kwa vyombo husika kuhusu vitendo vinavyoweza kuhatarisha usalama.
