TMA Yatoa Tahadhari ya Mafuriko, Yaweka Wazi Utabiri wa Mvua za Msimu (2026–2027)

Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA) imetoa utabiri wa msimu wa mvua unaoanzia mwezi Novemba 2026 hadi Aprili 2027, ikionya uwepo wa mvua za wastani hadi juu ya wastani katika maeneo mbalimbali nchini.

Katika taarifa hiyo iliyotolewa rasmi tarehe 23 Oktoba 2026, TMA imetoa tahadhari ya athari zinazoweza kujitokeza, zikiwemo mafuriko, uharibifu wa miundombinu, pamoja na milipuko ya magonjwa.

Mvua Kubwa Zaidi Novemba hadi Januari

Akizungumza wakati wa kutoa utabiri huo, Mkurugenzi wa TMA, Dk. Ladslaus Chang’a, ameeleza kuwa mvua nyingi zaidi zinatarajiwa kuanguka kati ya mwezi Novemba 2026 na Januari 2027, ikilinganishwa na kipindi cha Februari hadi Aprili mwaka ujao.

Dk. Chang’a amebainisha kuwa mabadiliko haya yanachangiwa kwa kiasi kikubwa na uwepo wa hali ya El Niño yenye nguvu kubwa, inayosababishwa na ongezeko la joto la bahari katika eneo la tropiki ya kati ya Bahari ya Pasifiki.

Related Posts