Azam Yatozwa Faini Kwa Kufanya Vitendo vya Kishirikina

Kamati ya Uendeshaji na Usimamizi wa Ligi ya Bodi ya Ligi Kuu Tanzania (TPLB) imeitoza faini ya TZS milioni 5 klabu ya Azam FC kwa kosa la kufanya vitendo vinavyoashiria imani za kishirikina kwenye mchezo dhidi ya Mbeya City.

TPLB imesema kabla ya kuingia uwanjani kwa ajili mazoezi mepesi (warm up) aliingia mtu aliyevaa jezi ya Azam na kuanza kumwaga vimiminika kwenye mstari wa uwanja karibu na benchi la ufundi la Azam, kisha akafanya ishara ya kuita ndipo wachezaji wakaingia uwanjani.

Related Posts