
Kamati ya Uendeshaji na Usimamizi wa Ligi ya Bodi ya Ligi Kuu Tanzania (TPLB) imeitoza Simba SC faini TZS milioni 5 kwa kosa la waokota mipira wa timu hiyo kufanya vitendo vinavyoashiria imani za kishirikina kwenye mchezo dhidi ya Namungo FC.
TPLB imesema wakati wa mchezo huo, watoto hao walionekana wakimwaga maji nyuma ya goli la timu ya Namungo, kitendo kinachoashiria imani za kishirikina.
