
Yanga Yapigwa Faina Mashabiki Kumrushia Chupa Kocha
Bodi ya Ligi Yamponda Yanga Faini ya Milioni 5 Kutokana na Vitendo vya Mashabiki
Dar es Salaam – Kamati ya Uendeshaji na Usimamizi wa Ligi ya Bodi ya Ligi Kuu Tanzania (TPLB) imemtoza klabu ya Yanga faini ya TZS milioni 5 (milioni tano za kitanzania).
Adhabu hiyo imetolewa kufuatia kosa la mashabiki wa klabu hiyo kumrushia chupa za maji kocha wa viungo wa klabu ya TRA United wakati wa mchezo wao wa Ligi.
Bodi hiyo imewakumbusha viongozi na wanachama wa klabu zote kuendelea kudhibiti mashabiki wao ili kuepuka adhabu za mara kwa mara zinazoweza kuathiri uendeshaji wa klabu na kuhatarisha usalama viwanjani.
