
Harambee Stars Yaibana Bafana Bafana Kufuzu AFCON 2027
Timu ya Taifa ya Kenya (Harambee Stars) imetoshana nguvu kwa sare ya mabao 2-2 ugenini dhidi ya Afrika Kusini (Bafana Bafana) katika mchezo wa Kundi D wa kufuzu fainali za AFCON 2027 uliochezwa Ijumaa, Novemba 13, 2026 katika Uwanja wa Orlando Amstel Arena jijini Johannesburg.
Matokeo hayo yanaifanya Afrika Kusini kuendelea kuongoza Kundi D ikiwa na alama 7 baada ya mechi tatu, huku Kenya ikiwa nafasi ya tatu, alama 2 kabla ya timu hizo kurudiana tena jijini Nairobi mnamo Jumanne, Novemba 17, 2026.
FT: Afrika Kusini πΏπ¦ 2-2 π°πͺ Kenya
β½ 08β Wanjala (OG)
β½ 77β Mofokeng
β½ 42β Olunga (P)
β½ 89β Ogam
