ALIYEKUWA beki wa kati wa Simba, raia wa DR Congo Henock Inonga ndiye nyota aliyefunga bao la mapema zaidi katika mechi tano zilizopita za Kariakoo Derby’ baina ya miamba hiyo kwenye ushindi wa kikosi hicho cha Msimbazi cha mabao 2-0.
.
Katika mechi hiyo iliyopigwa kwenye Uwanja wa Benjamin Mkapa, Yanga wakifanikiwa kuingiza timu uwanjani, Aprili 16, 2023, Inonga alifunga bao hilo dakika ya pili tu, huku Kibu Denis akitupia la pili dakika ya 32.

