Nature

Netanyahu Aapa Kulipiza Kisasi Kufuatia Shambulizi Kali la Iran Huko Israel

Waziri Mkuu wa Israel, Benjamin Netanyahu, amefanya ziara ya kushtukiza katika hospitali ya Soroka mjini Be’er Sheva kufuatia shambulio la kombora la ballistic lililotua moja kwa moja katika kituo hicho cha afya. Netanyahu, akiwa na sura ya uchungu na majonzi, alitembelea waathirika na kuzungumza kwa ukali kuhusu hatua ya Iran, akiitaja kuwa ni kitendo cha kigaidi kisichosameheka.

“Nipo hapa Soroka. Nimeambatana na Waziri wa Afya, Naibu Waziri Almon Kohen, na uongozi wa hospitali,” alisema Netanyahu mbele ya kamera huku akielekea moja kwa moja katika wodi za wagonjwa. “Tumepigwa katika sehemu ambayo hakuna hata mtu anayeweza kukimbia au kujilinda. Hii si vita ya kawaida, hii ni ugaidi wa wazi.”

Kwa mujibu wa Netanyahu, mashambulizi hayo yalilengwa katika maeneo nyeti na yasiyo ya kijeshi. Alieleza kuwa licha ya Israel kujibu kwa kulenga vituo vya nyuklia na makombora vya Iran, upande wa pili ulijibu kwa kushambulia hospitali, wodi za watoto na maeneo ya raia. “Hili linaonyesha tofauti ya wazi kati ya demokrasia inayozingatia sheria na magaidi wanaotaka kutuangamiza sote,” alisema kwa msisitizo.

Waziri Mkuu huyo aliwataka raia wote wa Israel kusimama pamoja na kuonyesha mshikamano wa kitaifa, akisisitiza kuwa hii ni vita ya uhai dhidi ya kifo, na ya haki dhidi ya uovu. “Hatutasita. Hili ni pigo, lakini hatutakubali. Lazima tupambane hadi mwisho. Lazima tuhakikishe haya hayaachi alama nyingine katika historia yetu,” alisema kwa sauti nzito.

Hii ni mara ya tatu kwa Netanyahu kutembelea maeneo yaliyoathiriwa moja kwa moja na mashambulizi ya Iran. Mbali na hospitali ya Soroka, alizuru pia maeneo ya makazi yaliyoathiriwa na makombora, na kisha kuelekea Telnof – kituo muhimu cha anga ambacho pia kililengwa katika mashambulizi ya hivi karibuni.

Katika ziara hiyo alifuatana na Waziri wa Ulinzi, Bwana Israwa CS, pamoja na Luteni Jenerali Aal Zamir, ambapo walikutana na maafisa wa jeshi na wapiganaji walioko mstari wa mbele. Viongozi hao walisisitiza kuwa hali iko mikononi mwao na kuwatia moyo askari waliopo vitani kuwa ushindi ni jambo lisiloepukika ikiwa mshikamano utaendelea.

Netanyahu alimaliza ziara yake kwa kusema wazi kuwa Israel itachukua hatua kali za kisasi na kuhakikisha Iran inabeba gharama ya kitendo hicho. “Huu ni wakati wa kuchukua hatua. Hatuwezi kuruhusu wauaji kuendesha dunia,” alihitimisha kwa sauti yenye machungu.

Mashambulizi haya yameibua taharuki si tu ndani ya Israel, bali pia katika jamii ya kimataifa, huku wengi wakihofia kuongezeka kwa mzozo wa Mashariki ya Kati hadi kufikia kiwango cha vita kubwa ya kikanda.

Related Posts

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *