Afisa Habari wa Azam FC Hasheem Ibwe leo amechukua fomu ya kutia nia ya kugombea Ubunge katika jimbo la Mwanga kwao Mkoani Kilimanjaro kupitia tiketi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM).
Ibwe ambaye kitaaluma ni Mwanahabari mbobevu aliyeitumikia tasnia ya habari kwa zaidi ya miaka 10, pia ni Mwanasiasa ambaye amekuwa akishiriki shughuli mbalimbali za kijamii na Chama nyumbani kwao Usangi Ndanda Mkoani Kilimanjaro.
Hasheem Ibwe amepata elimu yake ya Msingi katika Shule ya Msingi Kavazungu iliyopo Usangi Ndanda kuanzia mwaka 2000 na baadae kuhamia Dar es Salaam kwa ajili ya masomo ya elimu ya Sekondari aliyoyapata Alharamain Islamic Seminary na kisha kujiunga na Chuo cha Uandishi wa Habari Dar es Salaam (DSJ)

