Nature

Waumini 52 Waliokusanyika Ubungo Kibo Kwa Gwajima Wakamatwa

Jeshi la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam limeeleza kuwakamata na kuwashikilia watu 52 kwa ajili ya mahojiano kwa tuhuma za kufanya mkusanyiko wenye lengo la kufanya fujo eneo la Ubungo Kibo jijini Dar Es Salaam.

Taarifa iliyotolewa na Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar Es Salaam SACP Muliro Jumanne Muliro leo juni 29, 2025 imesema “watu hao walitokea kwenye Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Afrika Mashariki (KKAM) na walifanya ibada na wenzao lakini baada ya ibada kuisha wao wakaanza kutoka na kufanya vitendo hivyo vya fujo vilivyo kinyume na sheria.”

Taarifa hiyo imeongeza kuwa wahusika walitaka kufanya vurugu huku wakitaka kuingia kwenye barabara yanye magari mengi na kasi suala ambalo ni kinyume na sheria.

Pamoja na hayo Muliro ameeleza kuwa watuhumiwa wanahojiwa kwa kina na upelelezi unafanywa hatua zadi za kisheria zichukuliwe.

Hata hivyo ametoa onyo na kuwataka wananchi kufata sheria na kuepuka kufanya vitendo ambavyo vinaashiria au kusababisha vurugu..

Related Posts

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *