Nature

Kesi Mgawanyiko wa Rasilimali Chadema Kuendelea Leo

Kesi ya mgogoro wa mgawanyo wa rasilimali inayoikabili chama cha CHADEMA dhidi ya waliokuwa viongozi wa chama hicho inatarajiwa kuendelea leo katika Mahakama Kuu ya Tanzania, Masjala Ndogo ya Dar es Salaam.

Kesi hiyo ilifunguliwa na Said Issa Mohammed, Makamu Mwenyekiti mstaafu wa chama hicho, Zanzibar; Ahmed Rashid Khamid na Maulida Anna Komu ambao ni wajumbe wa Bodi ya Wadhamini wa chama hicho kutoka Zanzibar.

Awali kesi hiyo ya madai namba 8323 ya mwaka 2025 ilipangwa kusikilizwa Juni 24, 2025 lakini Jaji Hamidu Mwanga anayesikiliza kesi hiyo hakuwepo mahakamani ambapo iliahirishwa hadi leo Julai 10, 2025.

Itakumbukwa Juni 10, 2025 mahakama hiyo ilitoa zuio la muda kwa chama hicho kutofanya shughuli zozote za kichama hadi hapo kesi hiyo itakaposikilizwa.

Katika kesi hiyo wadai wanaiomba mahakama itamke na kuamuru amri za kutamka kuwa wadaiwa wamekiuka sheria zinazohusiana na vyama vya siasa na katiba ya chama hicho.

Pia wanadai kuna ubaguzi wa kidini na kijinsia, pamoja na kutoa maoni na matamko yaliyo na nia ya kuvuruga Muungano kati ya pande mbili za Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Related Posts

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *