Askofu mkuu wa makanisa ya Ufufuo na Uzima anayejulikana kwa majina ya Josephat Gwajima amevunja ukimya juu ya sababu zilizopelekea asigombee tena ubunge kuelekea katika uchaguzi mkuu wa mwaka huu.
Ikumbukwe kwamba Askofu Gwajima ni Mbunge mstaafu wa jimbo la Kawe lililopo mkoa wa Dar es Salaam na inaelezwa kwamba huyu ni moja kati ya viongozi waliofanya mambo makubwa sana ndani ya miaka mitano ambayo alikuwa madarakani.
Gwajima alikuwa anapigiwa hesabu za juu sana kwamba atagombea ubunge mwaka huu lakini mambo yamekuwa tofauti sana kwani kiongozi huyo hajaingia kwenye kinyang’anyilo cha kugombea tena nafasi hiyo.
Katika kuhakikisha kwamba anawatoa hofu wafuasi wake, Gwajima ameibuka na taarifa nzito inayoelezea sababu ambazo zimefanya asitie nia tena katika jimbo la Kawe kuelekea katika uchaguzi mkuu ambao utafanyika mwezi Oktoba mwaka huu.
Gazeti la Mwananchi la siku ya leo Jumatatu tarehe 28 Julai, limeweka wazi kwamba Gwajima amesema kwamba hajataka kugombea tena ubunge katika jimbo la Kawe kwa sababu anakipenda sana cheo chake cha kuwa Askofu wa makanisa ya Ufufuo na Uzima.
Gwajima ameachana na mpango wa kugombea tena nafasi ya Ubunge kwa sababu anaipenda sana kazi yake ya kuhubiri injili akiwa kama Askofu na pengine huu utakuwa ndio mwisho wake kwenye masuala ya siasa.
Kabla ya Gwajima kufanya maamuzi haya magumu, kulitokea jambo moja zito sana la kufungiwa kwa makanisa yake na sababu kubwa ilikuwa ni yeye kuchanganya mambo ya dini na siasa.
Askofu Josephat Gwajima pengine amejifunza kutokana na makosa na ndio maana amechagua kubaki na masuala ya kuhubiri dini pekee kwa maana ya kuachana na masuala ya siasa.

