Shirikisho la soka Afrika (CAF) limepanga kufanya droo ya hatua ya awali ya Michuano ya Ligi ya Mabingwa na Kombe la Shirikisho kwa msimu wa 2025-2026 jijini Dar es Salaam, Tanzania.
CAF imeamua kufanya droo hiyo kabla ya Agosti 12, 2025.
Awamu ya kwanza ya mechi za mashindano hayo itakuwa Septemba 19-21, 2025 huku mechi za marudiano ikiwa ni Septemba 26-28, 2025.

