Nature

CCM Ikienda Kwenye Uchaguzi Bila Reforms Itaangukia Pua

Askofu wa Makanisa ya Ufufuo na Uzima nchini na kada wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Josephat Gwajima, ameonya kuwa chama chochote kitakachopuuza maoni ya wananchi kitajikuta kinalia “kilio kisicho na mpangusa machozi.”

Akizungumza kupitia televisheni usiku wa siku ya Ijumaa, Gwajima ameishauri CCM kutoingia kwenye Uchaguzi Mkuu bila kwanza kushughulikia malalamiko na mpasuko uliopo miongoni mwa makundi ya wananchi.

“Msiingie kwenye uchaguzi bila kufanya damage control ya makundi haya. Makanisa yafunguliwe, wale walioumia watafuteni, zungumzeni nao. Rais ana nguvu ya kufanya hivyo,” amesema Gwajima.

Ameishauri Serikali na chama chake kufanya marekebisho madogo ya kisiasa (minimal reforms) ili kujenga mazingira jumuishi ya uchaguzi, ikiwemo kuruhusu wanasiasa wa upinzani kushiriki kikamilifu.

“CHADEMA si wanadai reforms? Kwanza mumuachie Tundu Lissu, mruhusu angalau minimal reforms ili wote waingie kwenye uchaguzi. Wapinzani wa Tanzania siyo shetani, siyo adui. Wanaishi kwa mujibu wa Katiba na ni Watanzania, na Tanzania ni yetu sote,” ameongeza Gwajima.

Source: Jambo TV

Related Posts