
Mfanyabiashara maarufu kutoka Uganda ambaye pia ni Mzazi mwenza wa Msanii Diamond Platnumz, amefunguka kuhusu tetesi zilizoenea mitandaoni zikimhusisha na kauli zinazodai kuwa Diamond hana uhakika wa ukoo wa baadhi ya Watoto wake.
Zari amedai kuwa Watoto wake wawili aliowazaa na Diamond, Princess Tiffah na Prince Nillan ni wa halili kwa Diamond bila shaka yoyote.
“Kwa sura tu, hakuna shaka Watoto wangu ni wa Diamond,” alisema Zari huku akikanusha vikali uvumi huo unaoendelea kusambazwa.
Aidha, Zari alieleza sababu ya yeye binafsi kutoambatana na Watoto hao kila wanapomtembelea Baba yao Nchini Tanzania, akifafanua kuwa sasa wamekua na wanaweza kusafiri wenyewe.
“Wamekua sasa, wanaweza kusafiri bila mimi. Na pia, kwa kuwa mimi ni Mke wa Bw. Lutaaya, siwezi kukutana na Diamond kibinafsi kwani ni kumkosea heshima Mume wangu wa sasa,” aliongeza Zari kwa uwazi.

