Nature

MARIOO Acharuka Kisa Inshu ya Kubadili Dini Kuwa Mkristo ili Amuoe PAULA

NYOTA wa muziki wa Bongo Fleva, Marioo ameshangaa wanaodai amebadili dini ili kufunga ndoa na Paula, jambo ambalo ameweka wazi sio rahisi kutokea kamwe.

Madai hayo yaliibuka wakati mkali huyo wa nyimbo kama ‘Hakuna Matata’ na ‘Mi Amor’ kumpeleka mchumba na mama watoto wake huyo, nyumbani kwao Arusha kusherehekea siku yake ya kuzaliwa.

Marioo alikanusha madai hayo na kusisitiza hawezi hawezi kufanya jambo hilo na watu wafahamu yeye ni Muislamu na hawezi kubadili imani yake hata kama ni kweli mapenzi huwa yana nguvu kubwa.

“Nawashangaa sana watu kila kukicha wananiuliza kama nimebadili dini, hakuna hata siku moja nimewahi kufanya hivyo, pia nilishawahi kuwaambia siwezi na sijawahi kujaribu kubadili na kwa nini nibadili dini ikiwa Paula ameshakubali kubadilisha dini?” alihoji Marioo.

Hata hivyo, kama itatokea Marioo kubadili dini haiwezi kuwa wa kwanza, kwani kuna baadhi ya wasanii na hata wanamichezo waliobadili dini zao za awali kwa sababu mbalimbali, ikiwamo hivi karibuni kipa wa zamani wa Simba, Yanga na Azam, Deogratius Munishi ‘Dida’ amedaiwa kubadili na kuitwa Yunus.

Related Posts