
Chama Cha Mapinduzi (CCM) kimemtangaza Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Kenny Kihongosi kuwa Katibu wa Itikadi, Uenezi wa Mafunzo wa chama hicho kuanzia Leo Agosti 23, 2025.
Uteuzi huo umetangazwa na mtangulizi wake Amos Makalla wakati wa mkutano na waandishi wa habari ambapo mbali na kumtangaza Kihongosi pia alitangaza majina ya wateuliwa wa kuombea ubunge kwa tiketi ya chama hicho sambamba na viongozi wengine wawili akiwemo Dkt. Asha-Rose Migiro ambaye amekuwa Katibu Mkuu wa CCM.

