Nature

TLS: Tutashirikiana na Poleple Kuhusu”Mifumo ya NIDA, INEC na CCM

Rais wa Chama cha Wanasheria Tanganyika (TLS) Wakili Boniface Mwabukusi

Rais wa Chama cha Wanasheria Tanganyika (TLS) Wakili Boniface Mwabukusi amesema chama hicho kipo tayari kushirikiana na aliyekuwa Balozi wa Tanzania Nchini Cuba, Humphrey kutokana na tuhuma alizotoa juu ya kuunganishwa kwa mifumo ya Vitambulisho vya Taifa (NIDA), Chama cha Mapinduzi(CCM) na Tume Huru ya Uchaguzi(INEC).

Mwabukusi amesema hayo leo Agosti 26, 2025 akieleza kuwa tuhuma alizotoa Polepole zinahitaji kuwa na uthibisho wa kitehama(IT) na endapo Polepole atawasilisha taarifa za kitaalam zinazothibitisha kuunganishwa kwa mifumo hiyo TLS itaanza kulishughulikia jambo hilo kisheria.

“yale maelezo ya Polepole ni mazuri lakini hayana ‘fact’ lazima atudadavulie zile ‘codes’ sisi kama TLS ni Wanasheria lakini sio wataalam Tehama(IT)” amesema Mwabukusi

“sisi TLS tunakunjua mikono kwa Mheshimwa Polepole asiogope anaweza akatumia namna yoyote ya faragha akatutumia zile taarifa ili tuweze kukaa na watalaam tuweze kuona hiki anachokiongea” ameongeza Mwabukusi

Aidha ameongeza kuwa endapo wakishafahamu namna mifumo hiyo inavyosomana watakuwa tayari kuchukua hatua za kisheria kuanzia hapo.

“Mimi namuomba Polepole tupo tayari kushiriki kuliendea hili jambo kisheria lakini kwa kupata hoja bora zaidi” – Mwabukusi

Related Posts