
Aliyekuwa Mbunge wa Jimbo la Mbulu Vijijini, Flatei Gregory Massay,amejiunga na ACT Wazalendo huku akichukua fomu ya kugombea Ubunge kupitia ACT Wazalendo
Fomu hiyo alikabidhiwa na Msimamizi wa Uchaguzi wa Jimbo la Mbulu Vijijini, Joseph Sambo, katika ofisi za Tume ya Taifa ya Uchaguzi.
ALSO READ | Bawacha ya Chadema Yamnyuka Pole Pole “Tuambie Aliyempiga Risasi Tundu Lissu”
Massay, ambaye aliwahi kulitumikia jimbo hilo katika Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia chama chake cha zamani (CCM) , anabaki kuwa miongoni mwa wanasiasa waliowahi kuvutia hisia za wananchi kutokana na namna yake ya kusisitiza hoja bungeni.
Ikumbukwe Mbunge huyu aliwahi kuruka sarakasi ndani ya ukumbi wa Bunge akipinga ucheleweshaji wa ujenzi wa barabara ya Mbulu–Haidom, iliyokuwa imeahidiwa na Wizara ya Ujenzi na Uchukuzi bila utekelezaji.

