
Mgombea wa Urais kupitia ACT Wazalendo, Luhaga Mpina amepoteza sifa za kugombea Urais kupitia tiketi ya ACT kwa kile kilichodaiwa kuwa mchakato wa uteuzi wake haujafuata katiba ya Chama hicho.
Hatua hiyo imepelekea Ofisi ya Msajili wa Vyama vya Siasa kubatilisha uteuzi wake kama mgombea wa Urais wa Tanzania kupitia Chama cha ACT Wazalendo, ikisema amekosa sifa za kuwa mgombea wa nafasi hiyo.

