Nature

TANZIA: Sheikh Rashid Njuki Afariki Dunia, Inadaiwa Alisomewa Albadil Apate Ajali ya Gari

Sheikh maarufu Rashid Njuki amefariki dunia usiku wa kuamkia leo baada ya kupata ajali ya gari. Tukio hili limetikisa jamii ya Kiislamu nchini na kuibua maswali mazito baada ya kusambaa kwa sauti na ushuhuda kwamba Sheikh huyo alifanyiwa Albadil (Dua ya mabaya) na baadhi ya wenzake waliokuwa wakipingana naye.

Tazama VIDEO Sheikh Njuki Akisomewa Albadiri:

Katika sauti hiyo, Sheikh Njuki mwenyewe alieleza wazi wazi kuwa alifanyiwa Dua maalum iliyolenga apate ajali ili taasisi yake ya Manasik ife. Na kwenye hiyo video Kuna mmoja alifanikiwa kuingia Dua iliposomwa na akarekodi.

Hali hii imechochea hisia kali mitandaoni na mijadala mikubwa kuhusu nafasi ya maombi ya mabaya ndani ya dini hii, nimewahi kuleta sana masomo na makala kuhusu hii dini inayotumia Majini kuua ,n k

Sheikh Njuki amezikwa leo jioni katika Mkoa wa Manyara mara baada ya Swala ya Magharibi, kwa wingi wa waumini, ndugu na marafiki waliomiminika kumuaga safari yake ya mwisho.

Mazishi yake yameacha simanzi kubwa, huku wengi wakitafakari kauli yake ya mwisho kuhusu Dua aliyosomewa, ambayo leo imetimia kwa njia ile ile aliyotabiriwa ( ajali ya gari.)

TAASISI YA MANASIK

Taasisi ya Manasik, iliyoanzishwa na Sheikh Njuki, ilikuwa na jukumu kubwa la kufundisha Waislamu taratibu za Hija na Umra kwa vitendo.

Ilitoa elimu kwa waumini wanaojiandaa kuelekea Makka, ikiwafundisha namna ya kutekeleza ibada mbalimbali kama tawaf, sa’i, wukufu Arafah na kurusha mawe (jamaraat),

Ilikuwa ikitambuliwa kama kituo maalum cha semina, mihadhara na mafunzo ya Hija kwa njia rahisi na za kisasa.

Kwa muda mfupi tu, taasisi hii ilianza kupata umaarufu mkubwa, ikivutia waumini kutoka maeneo mbalimbali nchini., huyu jamaa akaanza kupata pesa ,kwahiyo chanzo ni CHUKI

KWANINI ILIPIGWA VITA?

  1. Wivu na Ushawishi Umaarufu wa Sheikh Njuki na taasisi yake ulionekana tishio kwa madrasa na taasisi nyingine zilizokuwa zikijihusisha na elimu ya Hija na Umra.,(kumbuka hijja na Umra ni biashara za watu)
  2. Tofauti za Kiiitikadi – Wapo masheikh na walimu waliokuwa na mitazamo tofauti ya kifiqhi. Tofauti hizo zilipelekea kumtazama kama mpinzani na sio mshirika.,
  3. Hofu ya Kupoteza Wafuasi – Kadri waumini walivyoelekea kwenye Manasik, baadhi ya viongozi wengine waliamini kuwa ushawishi wao na nafasi zao kijamii vitadhoofika.,Kumbuka hii ni biashara kama biashara nyingine ,hivo wanaibiana wateja(maamuma)
  4. Fitna na Mashindano – Badala ya mshikamano, chuki binafsi na mashindano ya kijamii yakawa chanzo cha maombi ya mabaya. Hatimaye Sheikh Njuki akajikuta akifanyiwa Albadil Dua ya kumuombea apate ajali ili kuua taasisi yake.

Pumzika kwa Amani Sheikh Njuki

Related Posts