BREAKING NEWS: Yanga Yampiku Simba, Yamtambulisha Seleman Mwalimu ‘Gomez’

BREAKING NEWS: Yanga Yampiku Simba, Yamtambulisha Seleman Mwalimu 'Gomez'
BREAKING NEWS: Yanga Yampiku Simba, Yamtambulisha Seleman Mwalimu ‘Gomez’

VITA YA USAJILI: Yanga Yampiku Simba, Yamtambulisha Seleman Mwalimu ‘Gomez’

DAR ES SALAAM – Klabu ya Young Africans SC (Wananchi) imezua taharuki katika soko la usajili baada ya kumtambulisha rasmi mshambuliaji wa Kimataifa wa Tanzania, Selemani Mwalimu ‘Gomez’, kuwa mchezaji wao mpya kuelekea msimu wa 2026/27.

Usajili huu unakuja ikiwa ni siku chache tu tangu watani wao wa jadi, Simba SC, kutangaza kuwa walikuwa wamefikia makubaliano na klabu ya Wydad Casablanca ya Morocco kuhusu usajili wa mchezaji huyo.

Kwenye kilele cha tamasha la Simba Day (Agosti 8, 2026), Meneja wa Habari na Mawasiliano wa Simba SC alileta nafuu kwa mashabiki wa Msimbazi kwa kuthibitisha kuwa Gomez ni mali yao na alikuwa tayari yupo angani akirejea nchini kutokea Morocco.

Hata hivyo, Rais wa Yanga, Eng. Hersi Said, ameonekana kufanya ‘pindua meza’ ya kimya kimya na kukamilisha dili hilo, hatua inayozua mjadala mzito juu ya hatma ya kisheria na umiliki halali wa mshambuliaji huyo.

Related Posts