Nature

El Mando Aisifia Show ya Zuchu Yanga Day “Kafuta Makosa Aliyoyafanya Fainali CHAN”

WOW WHAT A SHOW BRO🤭🙌 Aisee sikutegemea kama Zuhura atafanya Show kali kama hii🙌

Zuchu kafanya kila kitu kinachofanya Show iitwe Kali, Kama Ubunifu kafanya, Ujasiri Jukwaani, Kumiliki Jukwaa, Connection na Mashabiki 🙌

Unajua ili Show iitwe kali ina vigezo vyake kwa upande wa Msanii, Msanii akitumiza hivo vigezo basi Show inaitwa Show kali, Kesho ntawaelezea na kuwaewesha yote kwenye RECAP & MANDO.

Tukubali tukatae Zuchu kapiga Show moja kali sanaa, kwanza Hizo Stage zake zilivyokuwa vinavadilishwa🙌

Huyu Binti alijipanga sana, Kafanya Show kali sana narudia Zuchu kapiga Show kaliii🙌

Ukitaka kuona hilo angalia namna alivyokuwa anabadili Stage zake halafu za kutengeneza🙌

Kwa HESHIMA ya hizi SHOW za Simba na Yanga kesho nafanya RECAP & MANDO SPECIAL siwezi kusubiri mpaka Jumatatu.

Neno moja la kuwaachia Wasanii wetu siku hizi Wanawekeza mnooo, haya ndio maendeleo ya muziki wetu.

Kingine Tusipende Kukariri wasanii waliotumbuiza Simba day na Yanga day wametupa Show kali sana bila Diamond, Alikiba, Harmonize wala Rayvanny.

Tuwaamini vijana wanaweza sanaa.

Neno moja tu kwa Meneja wa Zuchu Kim Kyando, futa maneno yako kwamba Viwanja vyetu miundombinu hairuhusu wasanii kupiga Show kali.

Sauti ipo poa, Msanii anamiliki Jukwaa, Kaweza ku-connect na Mashabiki, Kaimba LIVE licha ya kuwa ni ya STUDIO ila kaifanyia mazoezi ya kutosha.

Zuchu kafuta makosa yake ya CHAN.

Hii leo aliyoifanya Zuchu ni nini?? Kila kitu kipo Paerfect ingawa mapungufu machache tu.

Tukutane kesho kwenye @recap_mando ntawaeleza Ipi Show kali kati ya SIMBA DAY & YANGA DAY yaani MBOSSO & ZUCHU halafu MAPUNGUFU yao wote🤞

Najua wengi walikuwa wanasubiria niseme Show ya Zuchu mbaya, Sio kweli Show kali kesho ntaeleza utofauti wa Zuchu na Mbosso

Related Posts