
Moto mkubwa ulizuka na kuteketeza Soko Kuu la Kawe lililopo eneo Ukwamani, kuanzia mida ya usiku wa saa kuamkia leo.
Kwa mujibu wa mashuhuda wamesema, Jeshi la Zimamoto na Uokoaji lilifika eneo la tukio mara baada ya taarifa kutolewa na walijitahidi kuokoa baadhi ya mali lakini asilimia 70 ya mali zimeteketea kwa moto huo.
Chanzo cha moto huo hakijafahamika mpaka muda huu.

