
Kwa mujibu wa waziri Gwajima …………………………………….
“Ahsante kwa ushirikiano, mama mjane amenitumia sms, nikampigia, nikamsikiliza. Kifupi amesema, mwanasheria anaye, kesi iko Polisi na pia Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni anajua jambo hili.
Hata hivyo, changamoto zilizotokea ni huko kuvamiwa ghafla bila taarifa na kinyume na utaratibu stahiki wa kisheria ukizingatia kuwa, kesi iko Polisi. Hivyo, msaada wa haraka anaohitaji ni ulinzi wake na mali zake na dhidi ya hayo matishio anayopata.
HATUA: Nimewasiliana na Mhe. Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni na RPC Kinondoni na kuomba, wafanye hatua stahiki ili, mama mjane kwanza awe salama na utulivu kisha, hayo ya kisheria yaendelee kwa mujibu wa sheria ambapo, viongozi wote hao wamepokea kwa hatua stahiki.
Aidha, saa 9.11 jioni, nimeongea tena na mama mjane ambapo, ameniambia ni kweli Polisi walienda na wale waliokuwa wanamfanyia vurugu walitawanyika na sasa hali iko kwenye utulivu.
WITO KWA WANAODAI KUNUNUA NYUMBA YA MJANE:
Ndugu, hata kama mnadaiana, tafadhali fuateni taratibu halali za kisheria kupitia kwa mwanasheria wa mjane huyu. Hata katika mapito ya kisheria, tafadhali kumbukeni kuwa na subra na utu uwe kwanza na hapo ndiyo kila mmoja atapata haki yake na Mwenyezi Mungu atapendezwa nanyi nyote na kuwabariki wote. Amina.
Ahsanteni kwa ushirikiano wenu. Tuendelee kushirikiana kuzuia changamoto za kijamii na kuibua zinapotokea na kuzipatia mwongozo stahiki kwa wakati. 🇹🇿”

