Nature

Majeraha Yamtoa Fei Toto Taifa Stars, Kelvin Nashon Achukua Nafasi yake

Kiungo wa klabu ya Pamba Jiji ya Mwanza Kelvin Nashon ameitwa katika kikosi cha timu ya Taifa Tanzania ‘Taifa Stars’ kuchukua nafasi ya kiungo wa Azam FC, Feisal Salum aliyepata majeraha.

Kocha wa kikosi hicho Miguel Gamondi amewaongeza wachezaji Idd Suleiman “Nado” na Kelvin Nashon kwenye kikosi chake waliokwenda kuchukua nafasi za Feisal na Mudathir Yahya ambao wana majeruha.

Stars inajiandaa na mchezo wa kirafiki dhidi ya Kuwait utakaochezwa Novemba 15, 2025 Misri, huku kikosi hicho kikijiandaa na Mashindano ya AFCON, nchini Morocco, baadae Mwezi Desemba.

Related Posts