Aliyekuwa Mtendaji Mkuu wa zamani wa klabu za Simba SC ๐น๐ฟ na Yanga SC ๐น๐ฟ, Senzo Mbatha Mazingiza ๐ฟ๐ฆ, ametangazwa kuwa Mtendaji Mkuu mpya wa klabu ya TRA United FC ๐น๐ฟ.
Senzo, ambaye ana uzoefu mkubwa katika uongozi wa soka barani Afrika, amewahi kufanya kazi na vilabu vikubwa kama Yanga na Simba SC, ambako alisaidia kuimarisha miundombinu ya kiutawala na mafanikio ya ndani na kimataifa.
Ujio wake ndani ya TRA United unatarajiwa kuleta mabadiliko makubwa katika usimamizi wa klabu hiyo, hususa katika upande wa utawala na uendeshaji, huku lengo likiwa ni kuijenga timu hiyo kuwa miongoni mwa vilabu vinavyoshindana vikali kwenye ligi kuu ya NBC.
โฝ๐ฅ Karibu tena Tanzania Senzo Mbatha!
