Nature

Golikipa Camara Kupelekwa Morocco Kutibu Jeraha la Goti

Kwa mujibu wa taarifa kutoka klabu ya Simba, Mlinda mlango, Moussa Camara ataondoka kesho nchini kuelekea Morocco kwa ajili ya matibabu ya jeraha la goti yanayomsumbua.

Camara atafanyiwa upasuaji siku ya Jumatatu Novemba, 17 na anatarajiwa kuwa nje ya uwanja kwa takribani wiki nane mpaka 10.

Camara alipata majeraha hayo katika mchezo wa mkondo wa pili wa mtoano wa Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya Gaborone United uliopigwa Uwanja wa Benjamin Mkapa, Septemba 28.

Related Posts