BAADA ya kupoteza mechi yao ya kwanza ya hatua ya makundi msimu huu wa Ligi ya Mabingwa, Simba inahitaji ushindi wikiendi hii (Novemba 30) ili kurejesha ‘mzuka’ kikosini na hata kwa mashabiki.
Simba ikiwa ugenini nchini Mali, itashuka dimbani kumenyana na Stade Malien katika mchezo wa Kundi D.
Katika mechi ya kwanza ya Kundi hilo, ‘Wekundu wa Msimbazi’ walishindwa kunufaika na faida ya kucheza nyumbani kwani walifungwa bao 1-0 na Petro de Luanda ya Angola.
Ni siku ambayo Stade Malien ilipata sare ya bao 1-1 ikiwa ugenini dhidi ya Esperance de Tunis.
Ni kwa matokeo ya mechi hizo, sasa Petro iko kileleni ikiwa na pointi tatu, ikifuatiwa na Esperance na Stade Malien, ambazo kila moja ina pointi moja.
Kwamba katika Kundi hilo, Simba si tu iko mkiani, bali pia ndiyo timu pekee ambayo haijakusanya pointi.
Hata hivyo, endapo itashinda Jumapili, kisha Petro na Esperance zikatoa sare, basi Simba itasogea hadi nafasi ya pili, nyuma Waangola hao kwa tofauti ya pointi moja.
Ikumbukwe, Petro watakuwa katika Uwanja wao wa nyumbani, ambao walipoteza mechi mbili pekee kati ya 1 za Ligi Kuu ya Mali msimu uliopita.
Hivyo, endapo Simba itashinda na Petro kupata sare, Esperance na Stade Malien zitabaki katika nafasi ya tatu na ya nne zikiwa na pointi moja kila moja.
Ni kusema, bado Kundi hilo liko wazi kwa kila timu, ikizingatiwa kuwa ndiyo kwanza mzunguko wa pili unaanza.

