Aziz Ki akimbizwa hospitalini wakati wa mpambano wa ligi ya mashirikisho – Afrika
AmanisportsnewsNov 28, 2025Read original
Kiungo cha kati, mchezaji wa zamani wa Yanga SC Stephane Aziz Ki alikimbizwa hospitalini kwa huduma za dharura katika mchuano wa mashirikisho (CAFCC) barani Afrika nchini Tanzania, wakati Azam FC iliikaribisha Wydad Casablanca kwa mechi ya pili ya awamu ya makundi.
Mchezaji huyo raia wa Burkina Faso alijeruhiwa uwanjani jambo ambalo lililazimu kuondolewa akiwa katika hali mahututi na taarifa kutoka visiwa vya Zanzibar zimearifu kuwa anapokea matibabu katika hospitali moja iliyo karibu na uwanja wa Amaan.
Kiungo huyo ambaye anatarajiwa kutamba katika kipute cha AFCON mwezi ujao, hata hivyo amecheza dhidi ya Azam jumla ya mechi 8(bila ya kuhusisha ya leo) wakati huo akichezea Yanga SC kwenye ligi kuu ya soka nchini Tanzania. Wakati huo alifunga magoli 6 na kuchangia goli moja na kufunga hat trick moja.
Aidha mechi hiyo imekamilika kwa ushindi wa Wydad AC wa goli moja kwa nunge dhidi ya Azam FC.

