Waziri Mkuu Dkt. Mwigulu Nchemba amewasilisha ujumbe wa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan Kuelekea maadhimisho ya miaka 64 ya Uhuru ambapo amesema Kuwa kwa wale ambao hawana ulazima wa kwenda makazini waadhimishe sikukuu hiyo wakiwa majumbani.
Dkt. Nchemba amewasilisha ujumbe huo hii leo Disemba 8, 2025 ambapo amesema “Ndugu Wananchi Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh. Dkt. Samia Suluhu Hassan anawatakiwa Watanzania wote sikukuu ya Uhuru wa Tanzania inayoadhimishwa kila mwaka Tarehe 9, Disemba kila mwaka”
Aidha Serikali inawashauri Wananchi wote ambao Disemba 9, 2025 hawatokuw ana dharura kuitumia siku hiyo kwa mapumziko hivyo kusherehekea siku hiyo wakiwa nyumbani isipokuwa wale ambao majukumu yao yatawahitaji kuwepo kwenye vituo vyao vya kazi

