Msanii wa muziki wa Hiphop Emmanuel Elibariki(Nay wa Mitego) amesema hali ya kukataliwa kwa wasanii na mashabiki nchini ni jambo ambalo litatoa somo kwa wasanii kuwa wanapaswa kuwa sauti ya mashabiki/wananchi angalau mara chache.
Kupitia ukurasa wake wa Instagram Nay amechapisha video yake aliyokuwa akitoa wito kwa wasanii kujitoa na kuwasemea wananchi huku akitolea mfano wa wasanii wa mataifa kama Kenya na Nigeria ambao wapo wamekuwa wakiungana na wananchi pindi wanapowasilisha madai yao.
Ameambatanisha video hiyo na andiko akisema “Niliwashauri wasanii wenzangu kujitoa kwa wananchi wetu ata mara moja tu kwa mwaka kuwasemea kwa sababu wao ndo maboss wetu wa kwanza na ndio wenye hatma ya nguvu thamani na ushwishi tulio nao”
Nay ameongeza “tatizo kubwa la Mastar hapa nyumbani ni ubinafsi na kusahau maboss zetu ni hawa wananchi. Sasa maboss zetu now wameamua kutuonyesha kwamba wao ndio wanaotupa jeuri na maisha mazuri tuliyonayo Ni kwa sababu yao.
Aidha amesisitiza kuwa hatua ya watanzania sio la kulaumiwa bali kuchukuliwa kama somo kwa wasanii nchini “Mimi siwalaumu watanzania wana haki ya kuendelea na walichoamua npaka hasira zao zitakapoisha. Nadhani baada ya apo somo litakua limetuingia wasanii wote na tutakua tunaongea lugha moja wananchi na wasanii wote.”
