
Timu ya Mashabiki wa Simba FC imeifunga timu ya mashabiki ww Yanga FC magoli 2-0 katika mchezo wa kirafiki uliomalizika jioni ya leo katika Uwanja wa KMC complex.
Ofisa habari wa klabu ya Yanga Ali kamwe ambaye alikuwa sehemu ya benchi la ufundi na mchezaji pia amesema mchezo huo haujaisha maana klabu ya Simba waliingiza mamluki na mwamuzi hakuwa upande wao huku akisisitiza lazima mechi hiyo irudiwe maana hawajazoea unyonge.
Kwa upande wa Simba Afisa habari wa klabu hiyo Ahmed Ally ambaye alikuwa sehemu ya benchi la ufundi na mchezaji pia alikuwa sehemu ya ushindi amesema walikuja kucheza mechi ya ushindi sio ya heshima na wao ndio wabingwa wa mechi ya leo.
Baada ya mechi timu zote zilikabiziwa kiasi cha fedha Milioni Ishirini (20,000,000) huku Simba akikabiziwa na ubingwa wa mechi ya leo.
Lengo la mchezo huo uliovuta hisia za mashabiki wa mpira nchini ni kuwakutanisha pamoja mashabiki wa Simba na Yanga katika kudumisha umoja, upendo na mshikamano wa makundi hayo licha ya tofauti zao za kisoka.
