Mwakinyo ashinda kwa K.O, afichua siri

BONDIA Hassan Mwakinyo ameibuka mshindi kwa K.O dhidi ya mpinzani wake Stanley Eribo kutoka Nigeria, baada ya kumaliza pambano katika raundi mbili.

Pambano hilo limemalizika usiku huu katika ukumbi wa Warehouse Masaki, jijini Dar es Salaam.

Akizungumzia pambano hilo, Mwakinyo amesema imekuwa rahisi kwake kumshinda mpinzani wake kutokana na mazoezi anayofanya bila kujali ana mchezo au hana.

Amesema ubora wake haushuki hata akikaa muda mrefu bila kucheza kwa kuwa ameweka heshima katika mazoezi na anaamini ndiyo mhimili wa kazi yake.

Katika pambano lingine Mtanzania Hamadi Furahisha ameibuka mshindi kwa pointi dhidi ya Mmalawi Hanock Phiri katika pambano la raundi 10, huku Hassan Ndonga akimchapa Ismail Boyka.

Related Posts