MOROCCO: Timu ya Taifa ya #Tanzania “Taifa Stars” imeendeleza rekodi yake ya kutoshinda mchezo wa Michuano ya AFCON kwa kupata sare ya Goli 1-1 dhidi ya Uganda katika mchezo wa Kundi C.
Mchezo ujao wa Kundi, Tanzania itaivaa Tunisia wakati Uganda itacheza dhidi ya Nigeria, michezo yote ikichezwa Desemba 30, 2025.
Tanzania ilishiriki kwa mara ya kwanza michuano hiyo Mwaka 1980, kisha 2019 na 2024 ambapo haijawahi kushinda mchezo hata mmoja, ikifungwa mechi 7 na sare 3, mchezo wa Uganda unakuwa sare ya nne kwa jumla.
