Anthony Joshua, bondia maarufu wa Uingereza na Nigeria, amepata ajali ya barabarani katika eneo la Makun, jimbo la Ogun, nchini Nigeria. Ajali hiyo imetokea katika barabara kuu ya Lagos-Ibadan, ambapo gari lake aina ya Lexus Jeep liligongana na gari lingine ambalo lilikuwa limesimama.
Joshua alipata majeraha madogo, lakini watu wawili waliokuwa kwenye gari hilo wamefariki. Polisi ma mamlaka za afya wamethibitisha kuwa Joshua anaendelea vizuri.
