Diarra Namba Chafu, Adaka Penati Mbili Kuiwezesha Mali Kutinga Robo Fainali AFCON

PENALTI mbili alizookoa kipa wa Yanga, Djigui Diarra, zimemfanya apate TUZO ya Mchezaji Bora wa MECHI na zimeiwezesha timu yake ya taifa ya Mali kuing’oa Tunisia na kutinga hatua ya robo fainali ya michuano ya mwaka huu ya Mataifa ya Afrika (AFCON 2025).Mali wakiwa 10 kwa dakika zaidi ya 70 baada ya Woyo Coulibaly kulimwa kadi nyekundu dakika ya 26, bado walimudu kumaliza mchezo kwa sare ya bao 1-1.

Coulibaly alikumbana na adhabu hiyo baada ya rafu mbaya aliyomchezea staa wa Tunisia, Hannibal Mejbri.

Tunisia walikuwa wa kwanza kupata bao kupitia kwa Firas Chaouat, kisha Yassine Meriah kuisawazishia Mali kwa mkaju wa penalti iliyotokana na tukio la ‘kunawa’ mpira kwenye boksi.

Licha ya ubora wa Tunisia, Mali ilibaki imara na hatimaye kuibuka na ushindi wa penalti 3-2.

Diarra, ambaye alifanya kazi kubwa kwa dakika 90 na hata zile 30 za nyongeza, aliokoa penalti ya nne na ya tano kutoka kwa Elias Achouri na Mohamed Ali Ben Romdhane.

Mali waliweza kurudi mchezoni, licha ya nahodha wake, Yves Bissouma, kukosa penalti yao ya kwanza, kama ilivyokuwa kwa Nene Dorgeles aliyegongesha mwamba.

Kwa ushindi huo, sasa Mali watasafiri hadi mjini Tangier kuifuata Senegal kwa mchezo wa robo fainali utakaochezwa Ijumaa ya wiki ijayo.

Related Posts