Kwanza, nasikitishwa sana namna ambavyo ‘brand’ zetu wasanii wengi wa kike, zinahusishwa na mambo ya ugomvi, kusalitiana na mengine yasiyofaa. Wakati mwingine watu tu wametuvika vazi lisilovaa. Kwa vyovyote vile ifike mahali mambo haya yaishe, na tuwekeze kwenye kuheshimiana zaidi.
Kwa mantiki hiyo, jambo hili nitalisema leo kwa mara ya mwisho, ikiwa ni kwa sababu ya heshima ya mashabiki zangu na jamii yangu kwa ujumla. Mimi kama msanii ninayeheshimu jamii yangu, nyakati kama hizi nadhani nawajibika kueleza ukweli.
Iko hivi: Nimeona kwenye ukurasa wa Juma Lokole hapa instagram, ikipikwa kwamba “nimemzunguka rafiki yangu”. Ni kitu kibaya, cha hovyo, kimesemwa mara nyingi, nimeeleza ukweli mara nyingi lakini sijui kwa nini watu wanaendelea kulipotosha.
Kwa mara ya mwisho nasema: Whozu ni mwanamuziki kama mimi, na zaidi ya yote ni rafiki niliyefahamiana naye siku nyingi kabla ya yeye (Whozu) kuwa na mahusiano na “rafiki yangu”
Kwa bahati nzuri, rafiki zangu hao wawili walianza mahusiano, nikafurahi sana. Bahati mbaya katika kutofautiana kwao (ni kawaida kwenye mahusiano) kila mmoja ni kama alitaka niwe upande wake na mimi SIKUFANYA HIVYO, wote ni rafiki zangu.
Kilichotokea mara ya mwisho, mimi nilikuwa katika kupishana na rafiki yangu, na katika wakati huo nadhani hakuwa sawa saana na mpenzi wake Whozu. Nafikiri, rafiki huyu alitarajia mimi na Whozu hatutakuwa katika maelewano, kwa sababu zao ambazo wao.
Kwa ufupi: Mimi na Whozu hatukuwahi kuwa na mahusiano au jambo lolote la kimapenzi. Urafiki huu, haukuja baada ya mahusiano yake, hivyo hauwezi kufa kwa sababu zinazohusiana na hilo mahusiano Yao (Labda kama Whozu angekuwa amefanya jambo baya kama kumpiga mtu au lingine la kiunyanyasaji)
Mimi na aliyekuwa “rafiki yangu” tulipishana kwa sababu ya mambo mengine kabisa ambayo sioni haja ya kuzieleza mtandaoni (Hata hili nimelazimika kwa sababu naona jina langu linashambuliwa). Hili la Whozu naona ni katika kunitafutia ubaya tu mbele ya jamii, kama inavyosemwa kwamba “UKITAKA KUMUUA MBWA UNAMPA JINA BAYA”
Mwisho: Urafiki unaweza kufa, lakini usiwe mwanzo wa uadui. Kila mtu aendelee na maisha yake, bila sisi kutafutana ubaya.”
Ameandika Lulu Diva
